Maeneo ya Uwezeshaji ni yapi?

(i) Kuongeza Kasi ya Kukua kwa Uchumi na Kujenga Mazingira ya Uwekezaji kwa:

 • Kukuza Kipato cha Mtanzania ili kuinua ubora wa Maisha na kuandaa mazingira ya kibiashara ili yaweze kuharakisha kazi ya uwekezaji na kuongeza uzalishaji kwa ajili ya soko la ndani, kanda na soko la Dunia

(ii) Kuboresha Mfumo wa Utawala wa Sheria, Kodi na Huduma za Serikali kwa

 • Kuboresha mfumo na utawala wa kodi na utoaji wa leseni za biashara ili kuhamasisha uwekezaji
 • Kuimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma kwa umma kwa kutoa mafunzo, vitendea kazi bora na kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma

(iii) Upatikanaji wa Mitaji ya Wananchi kwa:

 • Kuandaa mpango mahususi wa kitaasisi utakaosaidia upatikanaji wa mikopo
 • Kuimarisha vyanzo vya akiba na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha Benki kukopesha kwa riba ndogo
 • Kujenga jamii inayokopesha kwa kutoa elimu ya kubuni na kusimamia miradi itakayoweza kuleta faida na kurejesha mikopo

(IV) Kuinua viwango vya ujuzi na uzoefu kwa Watanzania kwa:

 • Kurekebisha Mitaala ili kutoa elimu na ujuzi wa ujasiriamali na kuondoa mila na desturi potofu zisizo na upeo wa maendeleo
 • Kuwa na mfumo wa elimu utakaojenga misingi ya maendeleo ya ujasiriamali yanayokidhi mahitaji ya soko la ushindani

(V) Miundombinu ya Kiuchumi kwa:

Kutafuta rasilimali za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ili kuvutia uwekezaji na kuharakisha ukuaji wa uchumi

Kuweka mazingira yanayovutia Watanzania katika sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu

(VI) Ubinafsishaji kwa:

 • Kuwezesha ubunifu wa mikakati itakayotumika kuwasaidia Watanzania kumiliki mali na hisa kwenye mashirikia ya umma yaliyobinafsishwa.

(Vii) Masoko Kwa

 • Kuwezesha upatikanaji wa taarifa za masoko kwa wazalishaji wa bidhaa za Tanzania na kuendeleza soko la ndani;
 • Kuongeza kwa kasi mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Kimataifa kwa kusisitiza uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi viwango vya kimataifa.
 • Kuhamasisha uzuiaji wa kuwa soko la bidhaa mbovu kutoka nchi za nje na kuwezesha Watanzania kunufaika na zabuni zinazotolewa na Serikali

(viii) Ushirika kwa

Kuwezesha uanzishwaji wa vyama vya ushirikia madhubuti na kuimarika kwa vile vilivyopo

(ix) Ardhi kwa;

 • Kuwezesha Wananchi watumie Ardhi kama mtaji muhimu wa kuinua maisha yao ya Kiuchumi
 • Kupima maeneo na kuweka miundombinu inayohitajika kwa ajili ya kilimo, ufugaji, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi