Mh. Rais John Pombe Magufuli amemtua, Dkt. John Jingu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Dkt John Jingu ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Dkt. John Jingu (aliyesimama wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi alipotembelea ofisi za Baraza tarehe 30/12/2016.