Waratibu wa Uwezeshaji

Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi liliandaa mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi inatekelezwa kwa vitendo na wadau wote kutoka sekta za umma na sekta binafsi. Katika kuandaa Mkakati huo, Baraza liliandaa mwongozo wa utekelezaji na mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuanisha wadau, mfumo wa uratibu kitaifa na majukumu ya wadau mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa, kata, halmashauri, mikoa, wizara Taasisi na wakala mbalimbali wa huduma serikalini. Mwongozo huo unaelekeza kuanzishwa kwa kamati na madawati ya uwezeshaji .

Mpaka sasa madawati 26 katika mikoa na madawati 185 katika halmashauri zote Tanzania bara yameanzhishwa. Madawati haya yanafanya kazi ya kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uwezeshaji katika maeneo yao kwa kushirikiana na kamati za uwezeshaji zilizoanzishwa ambapo wadau kutoka sekta Binafsi wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa madawati (waratibu wa uwezeshaji) katika kutekeleza shughuli mbalimbali za uwezeshaji.

Pakua orodha ya waratibu wa uwezeshaji wa mikoa na wilaya