Habari

Imewekwa: Jun, 23 2021

ZIARA YA BARAZA LA UWEZESHAJI KIWANDA CHA POLYPET.

News Images

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi likiongozwa na Katibu Mtendaji Bibi Beng’i Issa latembelea kiwanda cha POLYPET kilichopo Mbezi Makonde, Jijini Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kinachojishughulisha na uzalishaji wa vifungashio vya chupa za aina mbalimbali na uzoefu wa kufanya kazi hiyo kwa miaka zaidi ya 11, kimeajili Watanzania wapatao 250.

Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Mtendaji wa NEEC alisema kiwanda hicho kimeingia mkataba na Taasisi ya SIDO ili kiweze kuwafikia wajasiriamali wadogo ambao shughuli zao zinahitaji vifungashio hivyo.

"Lengo la ziara yetu siku ya leo ni pamoja na kuwahakikishia Watanzania upatikanaji wa vifungashio ili kuondoa adha ya kutafuta bidhaa hizi katika Nchi za jirani" aliongeza Katibu Mtendaji

Mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya polypet Bw. Camil Dahood ametoa shukrani kwa kutembelewa na NEEC na amewakaribisha Wajasiriamali wenye uhitaji wa vifungashio vya bidhaa mbalimbali za kimiminika zikiwemo tomato sauce, maziwa, dawa, asali n.k

Aidha, Mkurugenzi huyo amewaalika Wafanyabiashara wabunifu wa vifungashio ili waweze kushauriana na kushirikiana katika kuboresha bidhaa hizo.