Ushiriki wa Watanzania

Imewekwa: Aug, 14 2019

Tangazo kwa Umma Kuhusu Maonesho ya Tatu ya Vikundi vya Kifedha, Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Tangazo kwa Umma Kuhusu Maonesho ya Tatu ya Vikundi vya Kifedha, Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeandaa Maonesho ya Tatu ya Vikundi vya Kifedha, Mifuko na Programu za Uwezeshaji wananchi Kiuchumi yatakayofanyika tarehe 14-20 Oktoba, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.

Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) na kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenister J.Mhagama (Mb).

Madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa kwa wananchi kuhusu uwepo, majukumu na vigezo vinavyotumika katika kutoa huduma za mifuko ya uwezeshaji ili kuwahamasisha wananchi kunufaika na fursa zilizopo katika mifuko hiyo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi mbalimbali yenye kuleta faida kupitia uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi vya kifedha vya kijamii.

Taasisi za umma na binafsi, taasisi za fedha, vikundi vya kifedha, mifuko ya uwezeshaji, program za uwezeshaji, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia pamoja na Wananchi mnaombwa kushiriki katika maonesho hayo kwa kupakuwa fomu ya maombi ya ushiriki inayopatikana katika tovuti ya Baraza Taifa la Uwezeshaji www.uwezeshaji.go.tz. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 05 Oktoba, 2019. Pakua fomu ya maombi ya ushiriki hapo chini.

Tangazo kwa Umma Kuhusu Maonesho ya Tatu ya Vikundi vya Kifedha, Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi