Wasifu

Festus Limbu

Festus Limbu

Ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Uchumi. Vilevile ni Mtafiti mwandamizi na Mshauri mwelekezi wa masuala ya uchumi chini ya Taasisi ya Utafiti (Economic and Social Research Foundation - ESRF). Mbunge Mstaafu wa jimbo la uchaguzi la Magu mkoani Mwanza (2000- 2015). Naibu Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo na Naibu waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya tatu. Aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (Tanzania Cotton Board) na kuwa mjumbe katika bodi mbalimbali hapa nchini, Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alimteua Dkt. Festus Limbu, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Septemba 2018.