Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
- Kuandaa Mpango Mkakati wa sekta na kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
- Kuhamasisha na kuhimiza ushirikishwaji makini wa wananchi katika shughuli za Kiuchumi
- Kusimamia, kuongoza na kubaini vyanzo vya kifedha kwa ajili ya mfuko wa mikopo/udhamini
- Kuandaa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya shughui za kiuchimi na mfumo wa menejimenti ya habari za uwezeshaji
- Kuhamasisha utafiti wa shughuli za Kiuchumi na kuhimiza ushirikiano ba nmashirikia ya kitafiti
- Kushirikiana na mashirika mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha uwezeshaji na upatikanaji wa huduma zinazohusiana na fursa za Kiuchumi
- Kuwezesha na kuratibu mafunzo ya mikopo na ujasiriamali kwa vikundi mbalimbali vya wananchi kutegemeana na mahitaji yao na changamoto zao
- Kuanzisha kanzidata ya kuwaunganisha watoa huduma na wazalishaji wa bidhaa za Tanzania na wawekezaji
- Kutoa muongozo wa ushirikishaji Wananchi kwenye miradi mikubwa ya uwekezaji
- Kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa namba kubwa ya vijana waliohitimu elimu ya juu
Miongoni mwa changamoto zinazokabili Baraza la Uwezeshaji katika utekelezaji wa majukumu yake ni pamoja na suala la mitazamo kuhusu uwezeshaji.Kuna uelewa mdogo kuhusu uwezeshaji ambapo wengi huamini ni fedha tu.
- Kuanzisha madawati ya Uwezeshaji kwenye halmashauri 186
- Uwepo wa siku ya VICOBA Tanzania
- Uelewa mpana wa wananchi kuhusiana na mifuko ya uwezeshaji na jinsi inavyofanya kazi.
- Kuanzishwa kwa mfuko wa MEF ambao moja kwa moja unasimamiwa na Baraza la Uwezeshaji
Baraza linawajibika katika kuitangaza mifuko hiyo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya vigezo vyake na namna inavyofanya kazi.
Mpaka hivi sasa kuna jumla ya Mifuko 45 ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikitoa dhamana za mikopo, mikopo na ruzuku.
Kwa kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa wazalishajimali ili waweze kuzalisha huduma na bidhaa ambazo zinaendana na soko la kimataifa na kunufaika na zabuni zinazotolewa na wawekezaji.
Baraza la Uwezeshaji linaratibu vikundi vya uwezeshaji kwa kupitia taasisi mwavuli ambazo zinasimamia zikiwemo VICOBA FETA, IR VICOBA na TIMAP
- Kupitia mifuko ya wanawake kwenye ngazi za halmashauri
- Kupitia mfuko wa Mwananchi Empowerement Fund ambao unafikia namba kubwa ya wanawake waliopo kwenye vikundi vya kifedha kama SACCOS na VICOBA
- Kupitia mafunzo ya ujasiriamali
- Kupitia mfuko wa Vijana wa YDF uliochini ya ofisi ya Waziri Mkuu
- Mifuko ya vijana iliyopo kwenye halmashauri zote
- Uwezeshaji kupitia mafunzo ya ujasiriamali kama Kijana Jiajiri na Kijana jiandalie ajira kwa ushirikiano na TECC.
- Programu za mafunzo na mitaji kwa wahitimu wa elimu ya juu (Young graduate Clinic)
- Program za mafunzo kwa vijana wa JKT