Kuratibu Ushiriki wa Watanzania Katika Uwezeshaji

Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji unaweza kufafanuliwa kama thamani ya ziada kwenye uchumi wa nchi unaotokana na umiliki na ushiriki wa wananchi katika ajira, manunuzi ya huduma na bidhaa, uhamisho wa teknolojia na kuongeza ujuzi kutokana na uwekezaji wa nje, mikataba ya kimataifa na uwekezaji mkubwa wa ndani.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lina mamlaka ya kuratibu, kuwezesha, na kutathmini kufuatilia maswala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.

Idara ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji inafanya kazi zifuatazo:

  • Kuratibu masuala ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi
  • Kutengeneza Mikakati na Miongozo ya utekelezaji wa Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji katika sekta mbalimbali
  • Kuwezesha ujengaji wa uwezo wa Kampuni za kitanzania na nguvu kazi kwa kushirikiana na wadau wengine
  • Kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wengine kutafiti juu ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji wa hapa nchini
  • Kufuatilia utekelezaji wa Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati katika sekta mbalimbali
  • Kuwezesha mafunzo ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kwa wadau mbalimbali
  • Kuratibu vikao vya wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa masuala ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji

Mafanikio:

  • Uwepo wa Waratibu wa Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji katika Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambao wapo 55 hadi sasa
  • Kuwezesha mafunzo ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kwa Waratibu na Wafanyakazi wa Baraza
  • Sera, Sheria na Kanuni za Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kutengwa katika sekta mbalimbali kama vile, Sera ya Nishati 2015, Sheria ya Mafuta 2015, Kanuni za Mafuta (Ushiriki wa Watanzania katika sekta ya Mafuta) 2017, Sheria ya Madini 2010 (iliyorekebishwa 2017) na Kanuni za Madini (Ushiriki wa Watanzania katika sekta ya Madini 2018)
  • Kuwajengea ufahamu wadau mbalimbali juu ya masuala ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji na fursa zilizopo katika miradi mikubwa ya uwekezaji inayotekelezwa nchini kupitia makongamano na warsha mbalimbali.
  • Kufanya tafiti bainifu kuhusu ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati kwenye sekta za Uziduaji, Uzalishaji, Kilimo na Ujenzi
  • Kufuatilia ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkatikati na uwekezaji unaofanyika nchini
  • Kufanya vikao vya wadau mbalimbali kuelezea changamoto zilizopo katika utekelezaji wa masuala ya ushiriki katika uwekezaji pamoja na kupokea maoni yao.