Wasifu

Timothy E. Simalenga

Timothy E. Simalenga

Ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St. John kilichopo Dodoma Tanzania tangu mwaka 2019. Pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya kusaidia Wananchi kujikwamua Kiuchumi (Social Economic Support Organization) tangu mwaka 2017. Aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha uratibu wa tafiti za maendeleo ya Kilimo katika ukanda wa Kusini mwa Afrika kuanzia mwaka 2012 mpaka 2016. Profesa Simalenga ni mtafiti mbobezi aliyeshika nafasi mbalimbali katika taasisi za utafiti ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 2012. Amekuwa mwalimu katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani ya na nje ya nchi kuanzia mwaka 1983 mpaka hivi sasa.