Wasifu

Nicodemus D. Mkama

Nicodemus D. Mkama

Ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji Tanzania (CMSA) tangu mwaka 2018, Ana uzoefu katika shughuli za masoko ya mitaji zaidi ya miaka 23. Kabla ya hapo alifanya kazi Benki Kuu ya Tanzania; Benki ya Eurafrican; na Taasisi ya Agakhan Foundation, International Organisation. CPA. Mkama ni mtaalamu mbobezi katika fani ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu anayetambuliwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA). Ni mtaalam mwelekezi (Consultant) katika uandaaji na ukaguzi wa hesabu katika viwango vya kitaifa na kimataifa.