Wasifu

Lucian A. Msambichaka

Lucian A. Msambichaka

Ni Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam katika masuala ya Uchumi wa kilimo. Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii(ISW) na ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara DCB. Alikuwa Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bodi ya Bima ya Afya(NHIF),Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bodi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Usihirika na Biashara(MUCCoBS),Moshi na Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kituo cha Ushauri cha Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA),Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji(TIC) na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA). Alikuwa Mshauri Mkuu na Mwezeshaji Kiongozi wa “Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Global Smart PartnershipDialogue)” na MshauriMkuu na Mwezeshaji Kiongozi wa “Majadiliano ya Kitaifa Kuhusu Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania”.