Kongamano la Uwezeshaji
Mahali |
Dodoma |
---|---|
Tarehe |
2019-06-15 - 2019-06-15 |
Muda |
08:00 Am - 05:00 Pm |
Madhumuni |
Kuzindua Ripoti ya Mwaka ya Uwezeshaji pamoja na kutambua michango ya wadau wa uwezeshaji waliofanya vizuri katika kuwezesha wananchi kiuchumi |
Event Contents |
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linatarajia kufanya Kongamano la nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tarehe 15 Juni 2019 Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau wasiopungua 300 kutoka kwenye sekta ya Umma na Binafsi nchini. Lengo la kongamano ni kukutanisha wadau wa sekta ya Umma na Binafsi kujadiliana masuala ya uwezeshaji kiuchumi, kujifunza toka kwa wadau wengine namna ya kuchochea juhudi za uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutambua Taasisi za Umma na Binafsi nchini zilizofanya vizuri katika kuratibu masuala ya uwezeshaji katika maeneo yao. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB). |
Washiriki |
Wadau mbalimbali wa Uwezeshaji kutoka Sekta ya Umma na Binafsi |
Ada ya Tukio |
Free |
Barua pepe |
neec@uwezeshaji.go.tz |