PIGA KURA KWA KUPENDEKEZA MJASIRIAMALI

PIGA KURA KWA KUPENDEKEZA MJASIRIAMALI

Mahali

ONLINE

Tarehe

2022-08-31 - 2022-09-07

Muda

31/08/2022 - 07/09/2022

Madhumuni

Mshindi TUZO ya UJASIRIAMALI

Event Contents

Kongamano la sita(6) la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linajumuisha utoaji wa tuzo kwa wadau waliofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wananchi kiuchumi katika mwaka 2021/2022. Tuzo hizi zitatolewa na Mgeni Rasmi - Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb).

Kati ya tuzo zitakazotolewa, ni tuzo za wajasiriamali ili kutambua mchango wao katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo mjumuisho na endelevu kupitia uwekezaji wanaoufanya.

Baraza, kupitia msimamizi na mshauri huru wa tuzo hizi kwa mwaka huu, Bridge Consult Limited, ambaye anasimamia mchakato wote wa kupata washindi, linawakaribisha wananchi, kama wadau wa maendeleo, kutoa mapendekezo ya wajasiriamali wanaostahili kupatiwa tuzo kwa kuzingatia mojawapo ya vigezo hivi.

1. Uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa kilimo

2. Ujumuishaji wa jinsia – wanawake, vijana, walemavu

3. Ujumuishaji wa vijiji

4. Utoaji wa elimu na mafunzo ili kutengeneza rasilimaliwatu

5. Utengenezaji wa ajira

6. Huduma za kifedha kwa makundi ambayo hayajaguswa vya kutosha

7. Kujali mabadiliko ya tabianchi

8. Utumiaji wa malighafi za ndani ya nchi

9. Mapato ya kifedha toka kwenye uwekezaji

10. Ina uvumbuzi na utumiaji wa teknolojia ya kisasa

Mjasiriamali atakayependekezwa mara nyingi ndiye atakayepatiwa tuzo. Mjasiriamali unaruhusiwa pia kujipendekeza.

Tafadhali bonyeza link hii ili kufanya mapendekezo ya tuzo za wajasiriamali

https://forms.gle/Kw9PiQzyXx3k4ejUA

Washiriki

Watu wote

Ada ya Tukio

NIL

Simu

+255222137362

Barua pepe

neec@uwezeshaji.go.tz