Wajasiriamali wanaweza kupata mikopo kwa haraka kwa kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa mtandao wa Baraza (NEMIS), kuwasiliana na mifuko na programu moja kwa moja au kutuma maombi yao kupitia anuani ya Posta ya Baraza inayopatikana katika tovuti. Hata hivyo, ni muhimu wajasiriamali waoneshe, ufahamu wa mipango yao ya biashara, na ufanisi wa shughuli zao ili kuongeza nafasi ya kupata mikopo kwa haraka.