Wajasiriamali wanapata taarifa kuhusu mifuko na programu za uwezeshaji kupitia njia mbalimbali ikiwemo kutembelea tovuti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), mfumo wa mtandao wa Baraza (NEMIS), semina, mafunzo au kufika makao makuu ya Ofisi za Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) zilizopo Jijini Dodoma.