Baraza linajitahidi kufikisha huduma za mifuko na programu za uwezeshaji kwa wajasiriamali wa maeneo ya vijijini kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya na mashirika yasiyo ya kiserikali. Hii inajumuisha mafunzo, huduma za kifedha, na mifumo ya usambazaji wa mikopo kwa maeneo ya mbali. Pia, Baraza limeanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo kila Halmashauri vinapatikana ambavyo vinatoa elimu ya fursa zilizopo katika mifuko na programu za uwezeshaji.