Baraza linafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kufanya vikao na wajasiriamali pia linashirikiana na taasisi za kifedha na mifuko ya uwezeshaji kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanapata mikopo kwa urahisi kwa kutoa urahisi wa mchakato wa maombi, kuondoa vikwazo vya kifedha kama vile dhamana, na kutoa elimu kuhusu jinsi ya kutengeneza mipango ya biashara yenye ufanisi.