Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Baraza linahamasisha na kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu mifuko na programu za uwezeshaji zilizopo. Pia, linatoa taarifa sahihi kuhusu vigezo na masharti ya mikopo ili wajasiriamali waweze kufikiwa na mifuko hii kwa urahisi na kuelewa jinsi ya kuitumia kwa ufanisi.