Baraza kwa kushirikiana na wadau linatoa mafunzo ya ujasiriamali, ushauri wa kifedha, na msaada wa kiufundi kwa wajasiriamali wanaoanzisha au kuendeleza biashara zao. Pia linashirikiana na taasisi nyingine kutoa elimu kuhusu namna ya kuandika mipango ya biashara na jinsi ya kufikia mifuko ya uwezeshaji.