Albamu ya Video
UZINDUZI WA KITABU CHA KANUNI 26 ZA MAFANIKIO
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng'i Issa, amezindua kitabu cha "Kanuni 26 za Mafanikio" kilichoandikwa na Bw. Mohamed Bassanga.
Imewekwa: Sep 10, 2020
ZIARA YA NEEC, MRADI WA KUFUA UMEME WA MWL. NYERERE (HYDRO POWER PROJECT)
Katibu Mtendaji wa @neec_uwezeshaji aliambatana na timu yake kutoka NEEC, katika kutembelea Mradi wa kufua umeme kwa maji uliopo Rufiji. ▪Dhamira ya ziara hii ni kujionea utekelezaji wa programu ya ushiriki wa Watanzania katika Mradi huu (Local Content) na kuona ni jinsi gani Wananchi wananufaika katika sekta ya Ajira, Ujuzi pamoja na uwekezaji wa Mradi kwenye Jamii - Corporate Social Responsibility (CSR). ▪Aidha Bi. Beng'i Issa ameshauri juu ya matumizi ya Tovuti mpya maalumu ya Local Content katika utangazaji wa fursa za ajira na zabuni zitakazojitokeza kwa Watanzania.
Imewekwa: Sep 10, 2020
MAONYESHO YA WANAWAKE WA KIAFRIKA 2020. "AFRICANWOMENSUCCESS"
Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng'i Issa amewahasa wanawake kujituma na kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za kibiashara kwani anaamini wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanikiwa na kuwa wakombozi katika familia zao na jamii kiujumla.
Imewekwa: Sep 10, 2020
ZIARA YA KUMTEMBELEA MJASIRIAMALI (MTANGA POLYMACHINERY) WILAYANI KIBAHA MKOANI PWANI.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Mhandisi Martine Ntemo ameongozana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng'i Issa pamoja na wadau wa kimaendeleo kutoka SIDO, SELF MICROFINANCE, BENKI YA AZANIA pamoja na watumishi wengine wa NEEC katika ziara ya tarehe 12/08/2020 ya kumtembelea Mjasiriamali mbunifu Bw. Heri Mtanga katika Kiwanda chake (Mtanga Polymachinery) kilichopo mtaa wa Twendepamoja kata ya Sofu, Wilayani Kibaha - Mkoani Pwani.
Imewekwa: Aug 26, 2020
Antony Mhanda - NEEC
Antony Mhanda - NEEC
Imewekwa: Jan 21, 2019
Baraza (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi kuendesha mafunzo ya ujasiriamali
Baraza (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi kuendesha mafunzo ya ujasiriamali
Imewekwa: Jan 21, 2019