Habari

Imewekwa: Jul, 05 2022

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lahitimisha ziara kukagua vituo vya uwezeshaji vilivyopo mkoani Dodoma

News Images

Hayo yamejiri leo ambapo watumishi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi wamehitimisha ziara ya kutembelea vituo vya Uwezeshaji katika Wilaya za Dodoma.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa wananchi kwenye miradi ya kimkakati Bi. Neema Mwakatobe akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Taasisi Bw. Gwakisa Bapala, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya @uwekezajiviwandabiashara Bi. Mwamini Mkwizu na baadhi ya watumishivitu @neec_uwezeshaji

Ujumbe huo ulikagua vituo vya Uwezeshaji vya Wilaya za Chamwino, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa, Chemba, Bahi na Dodoma jiji. Lengo kuu ni kuona huduma zipatikanazo katika vituo hivyo na kuona namna gani Baraza linaweza kushirikiana navyo ili kuboresha huduma za uwezeshaji na kuvisaidia katika sekta ya TEHAMA.