Habari

Imewekwa: Sep, 21 2020

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LASHIRIKI UZINDUZI WA MIRADI YA KISASA YA TAASISI YA UYACODE

News Images

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limeshiriki katika Mkutano Mkuu wa tatu wa Taasisi ya UYACODE uliofanyika Wilaya ya Chalinze kata ya Era kijiji cha Malivunde. Mkutano huo ulienda sambamba na uzinduzi wa miradi ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza aliweka jiwe la Msingi kuashiria kufunguliwa kwa miradi hiyo. Taasisi ya UYACODE ni Taasisi ambayo ina wavikundi wa VICOBA kutoka mikoa18 ya Tanzania bara na mitatu ya Zanzibar na imenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 2300 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kisasa. na Ujenzi wa Ofisi. Katibu Mtendaji aliishauri Taasisi hiyo kuhakikisha wanaifuata na kuitumia sheria ndogo ya huduma za fedha ya mwaka 2019 ambayyo imeanza kutekelezwa. Ikumbukwe kuwa kabla ya kutungwa kwa sheria ndogo Baraza limekuwa likilea vikundi vya VICOBA tangu mwaka 2011. Vile vile Katibu Mtendaji alipata fursa ya kutoa zawadi kwa wanavicoba ambao wamefanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja.