Habari

Imewekwa: Nov, 08 2022

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAWATAKA WADAU KUJIUNGA NA KANZIDATA YA UWEZESHAJI YA TAIFA

News Images

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng'i Issa amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Ofisi za Baraza viwanja vya Maonesho ya Nanenane - Dodoma.

Lengo kuu la Mkutano huo ni kuwajulisha wafanyabiashara, watoa huduma, makampuni, vikundi vidogo vya fedha na wawekezaji kuweza kujisajili katika mfumo huo wa kanzidata hiyo ambayo kwa sasa ipo hewani.

Kanzidata hiyo inatambulika kama "suppliers.uwezeshaji.go.tz" na ni bure kujiunga. "Kanzidata hii itawasaidia wawekezaji wa nje waweze kuona wafanyabiashara wa ndani ambao wanaweza kushirikiana katika miradi ya kimkakati" aliongeza Katibu Mtendaji.

Nae Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu Bw. Isaac Dirangw alisema kuwa mfumo huo ni rafiki kwa watumiaji lakini pia utasaidia hata vile vikundi vidogo kama mama lishe na kadhalika viweze kuinuka kiuchumi kwani kuwepo kwenye kanzidata hiyo kutawasaidia kuonekana kirahisi kwa ajili ya kuhusishwa kwenye miradi mbalimbali.