Habari

Imewekwa: Nov, 19 2020

KATIBU MTENDAJI WA NEEC AFUNGUA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA MKOANI GEITA

News Images

Ufunguzi huo umefanyika katika viwanja vya EPZ Ukumbi wa Nyerere eneo la Bombambili Mkoani Geita. Mgeni rasmiali kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng'i Issa, aliongozana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Bw. Denis Bandisa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) Bw. Richard Jordinson.

Akizungumza wakati wa ufunguzi Katibu Mtendaji alisema Baraza na Mgodi wa Dhahabu wa Geita wameingia makubaliano ya ushirikiano katika kutekeleza programu ya Uwezeshaji wakiwa na mategemeo makubwa kuwa program ya Uwezeshaji wakiwa na mategemeo makubwa kuwa program hii itawawezesha wafanyabiashara wa Geita kupata ujuzi utakao waongezea uwezo na stadi zitakazo wawezesha kushiriki na kushindana vema katika zabuni zinazotolewa na Mgodi pia.

"Nashukuru kwa kunialika na nawatakia ufuatiliaji mwema wa mafunzo pamoja na utekelezaji mzuri wa yale mliyofundishwa na mtakayofundishwa ili kuboresha Biashara zenu na hatimaye muweze kukuza uchumi wenu na wa Taifa kwa ujumla." Aliongeza Katibu Mtendaji.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita alisema kwa miaka mitatu GGML imefadhili miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 30 kwenye sekta mbalimbali kama Afya, Elimu na Miundo mbinu.

Vilevile alieleza kuwa nia ya GGML nikuendelea kuwa mshirika mzuri kwenye maendeleo ya wananchi muda wote wa uwekezaji na kuwa chachu kwa Serikali katika kufikia uchumi wakati mwaka 2025 na kuwezesha sekta ya madini kuchangia walau asilimia 10% yapato la Taifa.