Habari

Imewekwa: Mar, 03 2023

Katibu mtendaji wa NEEC Bibi Being'i Issa akitoa taarifa za maendeleo ya baraza na majukumu yake.

News Images

katibu mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(Bibi Being'i Issa) alizungumzia mambo mbalimbali yaliyofanywa na baraza katika kuwawezesha wananchi kiuchumi pamoja na kusimamia mifuko mbalimbali inayotoa mikopo kwa wananchi. Mifuko inayosimamiwa ni pamoja na inayotoa mikopo moja kwa moja, Mfano Women Development Fund, SELF Microfinance, inayotoa dhamana, Mfano PASS Trust, Mfuko wa Nishati Jadidifu na inayotoa ruzuku, Mfano TASAF, Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF).

Lakini pia Beng'i amesema NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) hapa wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa.

"NEEC hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini,"amesema.Zaidi ya Watanzania 83,000 wamepata ajira katika miradi ya kimkakati hapa nchini ambayo kwa hivi sasa Zaidi ya kamp[uni 1,770 za Kitanzanioa zimepata tenda katika miradi hiyo.