Habari

Imewekwa: Jul, 20 2022

Kikao cha nane (8) cha wadau wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha

News Images

Katibu Mtendaji wa NEEC Bibi Beng’i Issa ameongoza kikao cha nane (8) cha wadau wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha katika ukumbi wa mikutano wa NEEC.

Wadau hawa hukutana mara mbili (2) kila mwaka na kujadili mambo mbalimbali zikiwemo taarifa za taasisi mwamvuli za vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha, utekelezaji wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha, changamoto na mapendekezo ambayo yanalenga kuboresha huduma hizo.

Pamoja na mambo mengine wadau hawa wamepata elimu ya uwezeshaji kuhusu usajili wa watoa huduma za mafunzo na ushauri wa biashara (BDSPs) katika kanzidata ya uwezeshaji (NEED) pamoja na matumizi ya vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi.