Habari

Imewekwa: Jun, 23 2021

​KIWANDA CHAPIGA HATUA CHINI YA SANVN VIWANDA SCHEME

News Images

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi likiongozwa na Katibu Mtendaji Bibi Beng’i Issa latembelea kiwanda cha Bongo Toothpick kilichopo Bunju A Jijini Dar es Salaam, kiwanda hiki kinajishughulisha na uzalishaji wa vimbaka yaani Toothpick ni moja ya wanufaika wa programu ya SANVN VIWANDA SCHEME.

Katika ziara hiyo Katibu Mtendaji alisema vimbaka ni moja kati ya bidhaa ndogo ambayo Tanzania imekuwa ikiagiza kutoka nje ya Nchi, na lengo la SANVN VIWANDA SCHEME ni kuhakikisha bidhaa kama hizi zinazalishwa ndani ya Nchi na pengine kuziuza Nchi jirani.

Kupitia programu hii ya uendelezaji wa Viwanda vidogo na vya Kati, kiwanda cha Bongo Toothpick kimewezeshwa kupata mashine za kisasa ambazo zinatumika katika uzalishaji wa kiwango cha juu.

”Pamoja na kwamba Viwanda hivi vinarahisisha upatikanaji wa bidhaa za ndani zenye ubora vilevile vinazalisha ajira kwa Watanzania na kuongeza mapato ya Nchi kiujumla” aliongeza Beng’i Issa

Pamoja na mambo mengine Katibu Mtendaji alieleza kuwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linafanya jitihada za kuwaunganisha wajasiriamali hawa ili waweze kusambaza bidhaa zao katika miradi ya kimkakati, hii ni katika kutilia mkazo dhana ya ushiriki wa Watanzania katika Miradi yaani Local Content.

Kwa nafasi yake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bi. Violet Oscar amesema anaishukuru Serikali kupitia programu ya SANVN VIWANDA SCHEME ambayo imewezesha kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo.

“Mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa zetu tuliyapata miaka mitatu iliyopita, tukiwa na ndoto ya kumiliki kiwanda siku za usoni. Tunawashukuru SIDO kwa mafunzo hayo na baadae kutupa fursa ya kukuza ndoto yetu kupitia SANVN VIWANDA SCHEME” Bi. Violet Oscar

Aidha, Mjasiriamali huyo ametoa wito kwa Wanawake kuchukua hatua na kufanya maamuzi ya kijasiriliamali ili waweze kupiga hatua na kuboresha maisha yao na familia zao kiujumla.

Tanzania Census 2022