Habari

Imewekwa: Aug, 13 2019

Mafunzo ya vijana yazinduliwa Ruvuma

News Images

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Bibi Beng’i Issa amezindua mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara ambayo yanafanyika Ruvuma kwa awamu ya pili baada ya kuisha hivi karibuni Mjini Dodoma.

Imeelezwa kuwa mafunzo hayo ambayo yanahusisha pia watu wenye ulemavu yanatarajia kufikia vijana wasiopungua 150 huko Ruvuma.

Wakati wa uzinduzi Katibu Mtendaji alisema kuwa matarajio yake ni kuona vijana wanainuka kutoka hatua moja kwenda nyingine baada ya kupitia kwenye mafunzo haya ambayo yanaendeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Bunge, Sera, Vijana na wenye ulemavu kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji.

“Serikali ya Awamu ya tano imeleta mafunzo haya kwenu kwasababu inataka kuona yule mjasiriamali wa chini anasogea na kuwa mjasiriamali wa kati lakini hata yule wa kati nae anasogea na kuwa mjasiriaamali mkubwa”alisema Katibu Mtendaji.

“Katika mafunzo haya zipo taasisi za kifedha na zile za kurasimisha biashara hivyo mnapaswa kutumia fursa hii kunufaika na fursa za uwezeshaji ambazo zinapatikana Serikalini”aliongeza Bibi Beng’i Issa.

Katibu Mtendaji pia aliwataka vijana wa Ruvuma kuwa wabunifu na kutengeneza mazingira ya uaminifu kwa wateja wao na taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikitoa ruzuku na mikopo kwa vikundi vya uzalishajimali.

Mafunzo haya Kitaifa yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Jenista Mhagama Mjini Dodoma na yanatarajia kufanyika nchi nzima.