Habari

Imewekwa: Dec, 08 2022

Mafunzo ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

News Images

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lafanya mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi likiongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bibi Beng'i Issa leo limewapatia mafunzo wajumbe wa Baraza.

Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza Profesa Aurelia K. N. Kamuzora wamepata mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Mikutano wa Baraza, ofisi za Baraza makao makuu Dodoma.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwakumbusha juu ya majukumu ya Baraza lakini pia mambo ambayo wao kama wajumbe wanatakiwa kuyafanya ili kulisimamia vizuri Baraza liweze kuwahudumia Wananchi katika kuwawezesha Kiuchumi.