Habari

Imewekwa: May, 09 2022

MAONESHO YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI NI FURSA YA UKUAJI KIUCHUMI

News Images

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigella amewataka wananchi na wajasiriamali kutumia fursa za mifuko ya uwezeshaji na programu zake katika kuboresha uchumi wao.

"Maonesho haya ni sehemu ya masoko na ni fursa ya urasimishaji wa biashara, ni hatua katika uchumi" alisisitiza Shigella

Mkuu wa Mkoa amewahasa wananchi kuwekeza katika kilimo kwani Serikali ya awamu ya sita imefanya jitihada kubwa kuhakikisha wakulima wanapata masoko ndani na nje ya Nchi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa ametoa shukrani kwa @neec_uwezeshaji kwa kuchagua Mkoa wa Morogoro katika kanda ya hii ya Mashariki na amewataka wananchi hususan wa Mkoa wa Morogoro kushiriki kikamilifu.

Tanzania Census 2022