Habari

Imewekwa: Oct, 05 2021

MHE. WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA NA KUSIMAMIA VITUO VYA UWEZESHAJI.

News Images

Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa leo amewaagiza wakuu wa Mikoa kusimamia uanzishwaji wa vituo vya Uwezeshaji kwenye Halmashauri zao pamoja na kuvisimamia.

Mhe. Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji lililofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Mkoani Dodoma.

Sambamba na hayo Mhe. Kassim M. Majaliwa leo amezindua taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Uweshaji kwa mwaka wa fedha 2020/2021 katika ukumbi wa Mkoani humo.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi limehudhuriwa na Mawaziri mbali mbali, Makatibu wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Halmashauri za Dodoma, Taasisi za fedha, Taasisi binafsi na asasi za kiraia.

Kongamano hili ambalo limekutanisha wadau mbali mbali huku likiwa na lengo la kuchukua maoni kutoka kwa wadau mbali mbali kuboresha masuala mazima ya Uwezeshaji na hatimaye kuwainua wananchi kiuchumi.