Habari
Mkutano wa 16 wa Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi - Dodoma

Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi (VETA) Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na mifuko ya uwezeshaji, programu za uwezeshaji, Taasisi na Wizara zinazohusika moja kwa moja na masuala ya uwezeshaji wananchikiuchumi.
Mkutano huo ulioitishwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao ndio waratibu wa mifuko hiyo umeongozwa ma Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng'i Issa (M/Kiti).
Wajumbe wa mkutano huo walipata fursa ya kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za serikali na kuwekeana mikakati ya namna bora ya kusimamia uendeshaji wa mifuko pamoja na programu za uwezeshaji.
Sambamba na hilo wajumbe walifanya tathmini ya maonesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji yaliyofanyika Mwezi Mei 2022 Mkoani Morogoro kwa lengo la kuboresha maonesho yajayo yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2023.
Aidha, Katibu Mtendaji aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuwatakia utekelezaji mwema wa majukumu yao.
"Nawashukuru sana wajumbe kwa kujitokeza kwenu kwenye Mkutano huu. Niwaombe isiwe mwisho wa ushirikiano wetu na twende kuyatekeleza yale yote tuliyokubaliana" alisisitiza Katibu Mtendaji.