Habari

Imewekwa: Feb, 08 2021

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA ATEMBELEA VIWANJA VYA SHEIKH AMRI ABEID KUJIONEA MAONESHO YANAVYOENDELEA

News Images

Mhe. Kenani Kihongosi, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Leo ametembelea viwanja vya Sheikh Amri Abeid kujionea namna maonesho ya Mifuko na Program za Uwezeshaji yanavyoendelea.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ambaye alikuja kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Kimanta alitembelea mabanda mbali mbali ya Mifuko ya Uwezeshaji, Taasisi za Fedha, Taasisi za Umma na Wajasiriamali.

Uzinduzi rasmi wa maonesho hayo unatarajiwa kufanyika kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa.