Habari

Imewekwa: Jul, 19 2023

NEEC NA IFM WASAINI MKATABA WA HEET

News Images

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng'i Issa na Mkuu wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Prof. Josephat Lotto wakisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi Kiuchumi (HEET).

Katibu Mtendaji amesema kuwa makubaliano hayo yana tija hasa katika masuala ya kifedha kwani kila mwananchi anapaswa awe na ujuzi wa kutafuta fedha na kujua namna ya kuwekeza na kuzitunza ili aweze kukua kiuchumi.

Makubaliano haya yatasaidia kutoa mrejesho kwa Chuo kuhusu mambo gani yanapaswa kuingia katika mitaala yao ili kutoa vijana bora katika uchumi wa sasa.

Nae Prof. Lotto alisema kuwa makubaliano haya yatasaidia kuwawezesha kujua soko la ajira linataka nini ili kutengeneza mitaala itakayoendana na soko.

'Mradi huu una thamani ya dola milioni 10.5 na kiasi cha shilingi milioni 257 ni kwa ajili ya kuboresha Ushirikiano baina ya Taasisi hizi mbili.' alieleza Mkuu wa Chuo.