Habari

Imewekwa: Aug, 27 2020

NEEC YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA LIGHTWAY INITIATIVE.

News Images

Maadhimisho haya yamefanyika siku ya Jumatano; tarehe 26/08/2020 katika ukumbi wa Anatoglo uliopo Mnazi mmoja, Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Lightway Initiative Bw. Nichodemas Magele alifungua hafla hii kwa kuwa karibisha na kuwatambulisha waalikwa na wadhamini kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo NEEC, SIDO, NSSF, CRDB, AZANIA BANK, GS1 na MAI COLLECTION na walengwa wa kampeni ya “MSHIKE MKONO MJASIRIAMALI” ambao ni Wajasiriamali wenyewe.

Mkurugenzi wa Lightway Initiative; Bi Lightness Nkamba Budodi, aliwaalika wadhamini na Taasisi tajwa ili waweze kuwasalimia na kuwapa neon Wajasiriamali waliopata nafasi ya kushiriki katika siku hii maalumu;

Afisa Uwekezaji na Uwezeshaji; Bw. Omary Haji amesema Baraza liko kwa ajili ya kuhakikisha Wananchi wanakua Kiuchumi hivyo kupitia programu mbalimbali ambazo zinaendeshwa na NEEC kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa kimaendeleo.

Bw. Omary Haji aliongezea kwa kusema “kwa sasa tunaratibu programu ya uendelezaji wa viwanda vidogo na vya kati yani SANVN VIWANDA SCHEME ambayo imedhaminiwa na mfuko wa NSSF kwa kushirikiana na BENKI YA AZANIA, VETA na SIDO lengo likiwa ni kuendeleza viwanda vidogo na vya kati katika kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda”.

Kwa nafasi yake Mkurugenzi wa Lightway Initiative: Bi Lightness Budodi amesema anapenda kutumia siku hii kuzindua kampeni ya “MSHIKE MKONO MJASIRIAMALI” ambayo inalenga kuwasukuma Wajasiriamali kutoka katika hatua moja kwenda nyingine kwa kuwatafutia nafasi ya kupata ujuzi kutoka SIDO na kuwapatia vitendea kazi.

“Lightway Initiative tumekuwa daraja la Wajasiriamali katika kuhakikisha wanafanikisha malengo yao katika biashara zao” aliongezea Bi. Lightness.

Kwa kushirikiana naTaasisi za kiserikali sekta binafsi na wadau mbalimbali Lightway Initiative leo imetimiza mwaka mmoja tangu iwe rasmi na miaka mitatu ya kiutendaji hivyo nitoe shukrani za dhati kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wametupatia ushirikiano.

Kwa namna ya pekee naomba niwasilishe shukrani zangu kwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi – NEEC kwa kutushika mkono na kutuongoza, hivyo namshukuru sana Katibu Mtendaji Bi. Beng’i Issa kwa kutupokea kwa mikono miwili na kuhakikisha tunafanikisha shughuli za Lightway Initiative; aliongezea Bi. Lightness Budodi.

Mgeni Muhimu: DAS wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Seleman Makwiro awataka Wajasiriamali ambao bado hawajasajili vikundi vyao kufanya hivyo ili kurahisisha mchakato wa kupata Mikopo kwa ajili ya Vikundi inayotolewa na Serikali kwa lengo la kuwainua Wananchi Kiuchumi.

Mgeni Rasmi (kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa); Afisa Biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Thabit ameipongeza Taasisi ya Lightway Initiative kwa kufikisha mwaka mmoja katika shughuli zake za kiuwezeshaji.

Bw. Thabit amewahasa Wajasiriamali kuwa wabunifu kwani kupitia ubunifu huo wataweza kukua na kupata kipato cha ziada kutoka kwenye biashara hizo. Vilevile changamoto mbalimbali kama vile maeneo ya kufanya biashara pamoja na kukutanishwa na wadau wa kimaendeleo zitafanyiwa kazi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano chini ya Rais wake Dkt. John Pombe Magufuli imeandaa mikakati ya kuhakikisha inatengeneza mazingira bora ya kuendesha biashara Tanzania; aliongezea Afisa Biashara Mkoa

Mwisho kabisa Bi.Lightnness amemshukuru Mgeni Rasmi kwa kufanikisha sherehe ya siku hii maalumu kwa Lightway Initiative nawalengwa yaani Wajasiriamali.