Habari

Imewekwa: Dec, 18 2021

NEEC YATEMBELEA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI HOMBOLO - MAKULU JIJINI DODOMA.

News Images

Meneja wa Mifuko ya Uwezeshaji Bi. Nyakaho Mahemba akiambatana na baadhi ya watumishi wa NEEC walifanya ziara hiyo wakimuwakilisha katibu Mtendaji siku ya jana Tarehe 17/12/2021.

Vikundi hivyo vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ni Wando Farm, Kikundi cha chapakazi pamoja na Yamnyausi Organisation.

"Lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi hivyo ikiwa ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya shughuli hizo za kiuchumi" alisema Bi. Nyakaho

Vikundi hivyo vinafanya shughuli ya kilimo cha pilipili kichaa, pilipili mbuzi na arizeti pamoja na kuuza matofali ya kuchoma kwa ajili ya ujenzi.

Aidha, Mwenyekiti wa kikundi cha chapakazi kwa niaba ya vikundi vingine ameiomba serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji kutupia jicho shughuli zinazofanywa na wanakijiji kwani zinatija na zinahitaji uwezeshwaji kiuchumi.