Habari

Imewekwa: Sep, 16 2019

TAARIFA KWA UMMA

News Images

TAARIFA KWA UMMA

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia wadau wote wa Uwezeshaji kutoka kwenye Wizara, Idara, Taassi za Umma na Sekta binafsi kuhusu Kongamano la Kitaifa la ushiriki wa Wananchi katika miradi ya uwekezaji (Local Content) ambalo litafanyika tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa LAPF Mjini Dodoma na kushirikisha wadau zaidi ya 300.

Mgeni rasmi wa Kongamano hili anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa (MB) ambaye atazindua mwongozo wa Taifa wa ushiriki wa Wananchi katika miradi ya kimkakati na uwekezaji pamoja na Tovuti ya ushiriki wa Watanzania.

Kongamano la mwaka huu linabeba ujumbe wa ‘Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati,mafanikio, fursa na changamoto.

Wakati wa Kongamano kutakuwa na mada mbalimbali ambazo zitaibuliwa na waendesha mijadala ili kushirikishana uzoefu katika masuala ya ushirikishwaji wananchi kwenye miradi ya kimkakati.

Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi Lindi, mradi wa kufua umeme wa Nyerere, ujenzi wa barabara za Ubungo, Salender,barabara za Kuunganisha Mikoa, ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa Zahanati na vituo vya afya n.k.

Baraza linawakaribisha wadau wote wa uwezeshaji kuhudhuria kongamano hili lenye shabaha ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenye miradi ya kimkakati.

Imetolewa na;

Bi. Beng’i Issa

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

12 Sepemba, 2019