Habari

Imewekwa: Jul, 11 2021

​VIJANA WATAKIWA KUJIZATITI KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UJASIRIAMALI

News Images

Ameyasema hayo katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika uzinduzi wa programu ya kuwaendeleza vijana wajasiriamali ya KCB 2jiajiri uliofanyika Tarehe 05/07/2021, katika kumbi wa COSTECH Jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo Katibu Mtendaji amewapongeza Bank ya KCB ambao ndio wadhamini wa programu hii ambayo moja kwa moja inalenga kufungua fursa zaidi kwa vijana wa Kitanzania wenye fani mbalimbali.

“Nafahamu kwenye ujasiriamali kuna changamoto nyingi lakini niwasihi vijana msikate tamaa, mjue kabisa kuna kuanguka na kuinuka hivyo changamoto ni sehemu ya safari yenu ndefu ya Ujasiriamali” aliongeza Katibu Mtendaji

Kwa nafasi yake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Bw.Cosmas Kimario amesema programu hii itakayowagusa vijana wapatao 4000 Nchini ni mwanzo na hivyo Wajasiriamali wategemee makubwa zaidi kutoka KCB.

Bw. Cosmas amewataka Vijana Wajasiriamali kuanza polepole, akisisitiza kuwa ni vizuri kuwa na malengo ambayo wayafanyie kazi kwa hatua na nidhamu ya hali ya juu kwani hii itawasaidia katika ukuaji wa shughuli zao wakiwa na uzoefu wa hali ya juu.

Aidha, programu hii ya KCB 2jiajiri itafanyika katika mikoa 6 ikiwemo Mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Visiwani Zanzibar.