Habari

Imewekwa: Sep, 11 2020

WAJUMBE WA BARAZA LA TANO LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI WAPEWA SEMINA ELEKEZI

News Images

Wajumbe wa Baraza la tano (5) la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) wapatiwa Semina Elekezi (mafunzo) kutoka kwa Sekretarieti ya Baraza juu ya namna Baraza linavyotekeleza majukumu yake.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Kivukoni na kuongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza Bi. Beng'i Issa.

Katika Mafunzo hayo Mada mbali mbali ziliwasilishwa kwa wajumbe na kujadiliwa kwa kina..

Baadhi ya Mada zilizowasilishwa ni Majukumu ya Baraza, Programu za Uendeshaji, Mafanikio ya miaka mitatu iliyopita, Sera ya Taifa na Sheria ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Mpango Mkakati, Mwongozo wa Utendaji wa Baraza, Kanuni na Maadili za Baraza na nyinginezo.

Baada ya Mafunzo hayo wajumbe walifanya Uwasilisho kutokana na Mpango wa Uwezeshaji ambao uliwasilishwa na Mjumbe wa Baraza Prof. Timothy Simalenga.

Akiongea kwa niaba ya Menejimenti Katibu Mtendaji aliwashukuru wajumbe kwa kuhudhuria na kwa michango yao muhimu. ''Niwashukuru wajumbe kwa michango yenu muhimu na niahidi kuwa tutaenda kufanyia kazi michango yenu'' aliongeza Katibu Mtendaji.

Wakati akifunga Mwenyekiti wa Baraza Dr.Festus Limbu aliwashukuru wajumbe pamoja na Sekretarieti kwa kazi nzuri iliyofanywa katika Semina Elekezi hiyo na Uwasilishaji mzuri wa mada