Habari

Imewekwa: Sep, 03 2020

WARSHA YA KUTAMBULISHA NA KUTOA ELIMU YA MPANGO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KUPITIA MPANGO WA SANVN VIWANDA SCHEME.

News Images

Warsha hii ilifanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 03/09/2020 katika ukumbi wa NSSF – Mafao House uliopo Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es Salaam. Warsha hii imewakutanisha wawakilishi kutoka Taasisi zinazoshirikiana katika mpango huu wa SANVN VIWANDA SCHEME; ambazo ni SIDO, BENKI YA AZANIA, NEEC, VETA, NSSF na Wajasiriamali wa Viwanda kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la Warsha hii ni kutoa elimu kwa Wajasiriamali juu ya mpango wa uendelezaji wa Viwanda vidogo na vya kati SANVN VIWANDA SCHEME.

Mwakilishi kutoka NSSF Bw. John Mwalisu amesema katika mpango huu NSSF ipo kuhakikisha pesa zitakazokidhi mahitaji ya mikopo zinakuwepo ili wanachama wake waweze kukopa na lengo ni kukuza shughuli za kiuchumi ambazo zinafanywa na Wajasiriamali ambao ni wanachama au wanahitaji kuwa wanachama wa NSSF.

Bw. John Mwalisu aliongezea kwa kusema hapo baadae NSSF itaanza kutoa mafao vitu kwa wanachama wake ambapo kama gharama ni kubwa itakuwa kwa njia ya mkopo, kama ni ndogo itakuwa ni faida kwa mwanachama yaani hatotakiwa kufanyarejesho: mfano wa vitu hivyo kwa wakulima watapata mbegu, trekta, vifaa na vinginevyo.

Afisa Uwekezaji na Uwezeshaji Mwandamizi Kutoka NEEC Bw.. Mohamed Aziz, amesema Baraza lipo kwa ajili ya kuratibu, kusimamia na kufuatilia shughuli zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi. Hivyo ni waratibu wa mpango huu wa SANVN VIWANDA SCHEME ambaounalenga kuwawezesha Wajasiriamali wenye viwanda vidogo navya kati ambao dhumuni lake kuu ni kutatua changamoto ya mitaji.

Mwakilishi kutoka VETA Bw. Baraka Said Maridadi alielezea namna ya kuwasilisha maombi ya mkopo na nyaraka. Utaratibu utamtaka mjasiriamali kuandaa barua ya maombi ya mkopo na viambatanishi kishakufikisha katika ofisi zozote za Veta zilizopo karibu.

“Lengo ni kufanikisha wamiliki wa viwanda au wajasiriamali wanapata mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji pamoja na kuboresha maisha yao” alisema Bw. Maridadi

Mwakilishikutoka Benki ya Azania Bw.Thobias Samweli kutoka kitengo cha biashara rejareja, ameainisha aina za mikopo ambayo itatolewa katika mpango huu wa SANVN VIWANDA SCHEME. Mkopo wa kwanza ni wa vifaa: ambao utamtaka Mjasiriamali kuchangia 20% ya gharama za mashine ambapo benki itatoa 80% ambazo zitalipiwa moja kwa moja kwa msambazaji. Muda wa marejesho ni mpaka miaka 7 na riba ni asilimia 13 kwa njia ya reducing balance.

Mkopo mwingine ni wa kuendeshea mradi, huu mkopo ni kwa ajili ya Wajasiriamali ambao hawahitaji mashine wala mkopo wa muda mrefu hivyo muda wake ni miaka 3, huu mkopo unahitaji dhamana ambayo inatoshereza kiwango cha mkopo.

“Billioni 5 zimetolewa na NSSF kama kianzio katika hatua ya mwanzo ya utekelezaji wa mpango huu, Benki ya Azania itahakikisha mikopo hii inatoka kwa muda ili kuweza kutimiza ndoto za Wajasiriamali” aliongezea Bw. Thobias

Mwakilishi kutoka SIDO Bw. Baraka kandonga amesema Taasisi hiyoipo ili kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali ili kuwaandaa waweze kukopesheka yaani kuhakikishawanakidhi vigezo na sifa zinazohitajika katika mpango huu wa SANVN VIWANDA SCHEME.

Naye Bw. Mohamed Aziz wakati akifunga aliwashukuru Wajasiriamali wa viwanda kwa kujitokeza katik warsha hii na kuwahimiza kuchangamkia fursa iliyopo mbele yao.