Habari

Imewekwa: Jan, 21 2022

WARSHA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA GEITA - KATORO

News Images

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Wilson Shimo akifungua warsha ya wafanyabiashara Mkoa wa Geita inayofanyika leo (21/01/2021) katika ukumbi wa JJ Hotel - Katoro, Mkoa wa Geita.Katika ufunguzi huo Mhe. Shimo amewahasa wafanyabiashara kutumia fursa za warsha hizi kupata taarifa zitakazowawezesha kuboresha biashara zao na kupiga hatua kiuchumi, hii ni pamoja na kushiriki makongamano na kutembelea kituo cha uwezeshaji na taarifa kilichopo viwanja vya maonesho ya madini kata ya Bombambili katika Halmashauri ya Mji wa Geita.


Aidha, Mkuu wa Wilaya ametoa agizo kwa Baraza la uwezeshaji kwa kushirikiana na mgodi wa geita kuongeza juhudi katika kukitangaza kituo hicho hili wananchi wengi waweze kufahamu huduma zinazopatikana ili ziweze kuwawezesha kiuchumi.