Habari

Imewekwa: Jan, 20 2022

​WARSHA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA GEITA St. Aloycius - Shilabela

News Images

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Stak Senyamule amefungua warsha iliyowakutanisha Wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kujadili fursa za zabuni zitolewazo na @geitagoldmine

Mkuu wa Mkoa amewashukuru vongozi na washiriki wote kwa kuacha majukumu yao na kukubali kushiriki kikamilifu katika warsha hii yenye lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya fursa zilizopo katika Mkoa wa Geita na kipekee fursa za kibiashara zinazopatikana kupitia mgodi wa dhahabu wa Geita.

Aidha, Mhe. Sinyamule ametoa shukrani zake kwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kwa kuendelea kushirikiana kubuni kusimamia na kutekeleza mradi wa uendelezaji wa biashara kwa wajasiriamali wa mkoa wa Geita ambao umelenga kuwainua wananchi wa mkoa wa Geita na Taifa kiuchumi.