Habari
Waziri Mkuu amezitaka Wizara za Kisekta kuweka mipango madhubuti ya kiuwezeshaji
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa amezitaka Wizara za Kisekta kuweka mipango madhubuti ya kuyafikia makundi mbalimbali muhimu yenye uhitaji wa uwezeshwaji.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha kongamano la sita la uwezeshaji wananchi kiuchumi lililofanyika 19/09/2022, katika Ukumbi wa LAPF- Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu ametoa agizo kwa Mikoa kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi na ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa kwenda kujifunza kupitia kituo cha mfano cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichopo Mkoa wa Shinyanga (Kahama).
"Mikoa ambayo haijaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi, sasa ni wakati sahihi wa kuanzisha vituo hivyo" alisisitiza Mhe. Majaliwa
Kwa nafasi yake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara mbalimbali, Taasisi na wadau wa uwezeshaji kiujumla kwa kufanikisha kongamano la sita la uwezeshaji.
Aidha Katibu Mtendaji wa NEEC, Bibi Beng’i Issa amesema Baraza litaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau ili kuongeza kasi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi hapa nchini.