Habari

Imewekwa: Jan, 31 2020

Vijana Jijini Mwanza waelezwa juu ya Fursa zipatikanazo katika Mifuko ya Uwezeshaji, January 2020

News Images

Kongamano hilo limefanyika Jijini Mwanza katika ukumbi wa Mafunzo wa Benki kuu siku ya Jumamosi Tarehe 11/1/2020, lilifunguliwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi iuchumi Bi Beng’i M Issa. Limeandaliwa na UVCCM Mkoa wa mwanza na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na kuwezeshwa na wadau wa kimaendeleo Tanzania wakiwemo Manispaa ya Nyamagana, TBS, NSSF, BOT, SIDO, SELF MICROFINANCE, TADB, PASS TRUST, BRELA, OWM KVAU, TIB DEVELOPMENT na CRB.

Kongamano limelenga kuleta uelewa kwa vijana juu ya Mifuko ya Uwezeshaji, hii ni pamoja na umuhimu wa mifuko na faida zipatkanazo katika mifuko ya uwezeshaji kiujumla.

Katibu Mtenfaji wa Baraza la Uwezeshaji amewataka Vijana mkoani Mwanza wasisite kuchangamkia fursa zipatikanazo Mkoani humo kwani kupitia mifuko ya Uwezeshaji wanaweza kufanikisha malengo ya kibiashara waliyonayo hivyo wasiwe waoga kuihushisha mifuko katika hilo.

“Nawasihi sana Vijana wa Mkoani Mwanza, fursa ni nyingi Mwanza kuna ardhi nzuri pia kuna Ziwa Victoria na hizi ni fursa kwa jicho la harakalakinifursa ni nyingi sana hivyo msiwe ha hofu kuhusu mitaji cha msingi ni kufuata vigezo na masharti yanayotolewa na Mifuko ya Uwezesahaji kwani ipo kwa ajili yenu” Alisema Bi Beng’i Issa (Katibu Mtendaji NEEC).

Pamoja na hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi amewashukuru sana UVCCM Mkoani Mwanza kwa kutambua umuhimu wa Mifuko ua Uwezeshaji na kuona haja ya kuandaa Kongamano hilo linalowahussu Vijana. Ikiwa ni moja ya jitihada ya juu kabisa katika kusaidia Lengo la Sera ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Uchumi wa kati ya Viwanda.

Pia kwa namna ya pekee Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Mwanza, amewataka vijana wenzake kuna na wazo la kujiajiri kwani ujasiriamali ni mzuri hivyo watumie uwepo wa Mifuko ya Uwezeshaji ili kutimiza ndoto zao. Vilevile washirikiane na wadau wakuu wa Uwezeshaji nchini Tanzania yani Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kutimiza adhima ya kuwezeshwa Kiuchumi kwani walengwa ni Wananchi wa Tanzania hivyo wana kila sifa.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeona umuhimu wa kuandaa Makongamano mengi zaidi kuhusu Mifuko ya Uwezeshaji, kwa kushikiana na wadau wa kimaendeleo nchini Tanzania.