Habari

Imewekwa: Jun, 17 2021

ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU - NEEC

News Images

Mapema leo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu @owm_tz (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kasper Mmuya ametembelea Ofisi za Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) - Jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu amelitaka Baraza la Uwezeshaji kwa kushirikiana na wadau kuongeza jitihada katika kuwajengea uwezo Watanzania kwenye fani ambazo zinahitajika katika Miradi ya Kimkakati Nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wanakidhi vigezo vitakavyo wawezesha kupata nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika kujenga Uchumi wa Nchi na kuboresha maisha yao.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu amewahasa watumishi wa NEEC kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kufanya tathmini ya mikopo inayotolewa na Mifuko ya Uwezeshaji pamoja na kufuatilia Taarifa za Ushiriki wa Watanzania katika Miradi endelevu ikiwemo kutembelea maeneo hayo ili kujiridhisha.

Kwa nafasi yake Katibu Mtendaji wa NEEC Bibi Beng'i Issa amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kuweza kutenga muda wake na kutembelea Ofisi za Baraza la Uwezeshaji.