Mapitio ya Sheria

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ambacho ni chombo cha juu cha uratibu wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 kifungu namba 16 linawajibika moja kwa moja katika kufanya mapitio na maboresho ya sheria mbalimbali za nchi zinazohusiana na masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kutoa mapendekezo yatakayorahisisha utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji kwa Wizara, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi hapa nchini.

Katika kufanikisha utekelezaji wa sera ya uwezeshaji Baraza linashirikiana kwa karibu na Wizara, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ili kubaini vikwazo vilivyopo vikiwemo vile vya kisheria na kanuni na kutafuta suluhisho la pamoja katika kutatua changamoto zilizopo.

Baraza linawajibika katika kutoa mapendelezo yake juu ya mabadiliko ya kisheria kwa Taasisi husika ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na ushiriki wao katika miradi mbalimbali ya Kiuchumi.