Kusimamia Mifumo ya Habari ya Uwezeshaji

Moja ya majukumu ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji nikusimamia mifumo ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Mfumo wa Taarifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ni mfumo unaokusanya taarifa na habari za uwezeshaji na kuzisambaza kwa watumiaji wake (umma).

Mfumo wa Taarifa na Usimamizi ni mfumo unaokusanya, kuhifadhi, na kusambaza taarifa kwa njia ya habari zinazohitajika kutekeleza kazi za usimamizi.

Hivi sasa NEEC imeanzisha tovuti ya Uwezeshaji ambayo ina taarifa na habari mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi, hata hivyo, Baraza lina Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za kisekta kuhusu uwezeshaji wa wananchi kiuchumi nchini Tanzania. Sambamba na mfumo huo, mifumo mingine ambayo inaandaliwa ni:-

  • Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini
  • Kanzidata ya vikundi vya kijamii.
  • Kanzidata ya mifuko ya uwezeshaji.
  • Tovuti ya miradi mikubwa ya serikali.