Majukumu

  1. Kuandaa Mpango Mkakati wa sekta na kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi;
  2. Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji, na ushirikishwaji makini wa Wananchi kwenye shughuli za Kiuchumi;
  3. Kusimamia, kuongoza na kubaini vyanzo vya fedha kwa ajili ya mfuko wa mikopo/udhamini;
  4. Kuwezesha na kuratibu mafunzo ya mikopo na ujasiriamali kwa vikundi mbalimbali vya Wananchi kutegemeana na mahitaji yao na changamoto zao;
  5. Kushirikiana na mashirika mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha uwezeshaji na upatikanaji wa huduma zinazohusiana na fursa za kiuchumi;
  6. Kuhamasisha utafiti wa shughuli za kiuchumi na kuhimiza ushirikiano na mashirika ya kitafiti; na
  7. Kuandaa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya shughuli za kiuchumi na mfumo wa menejimenti ya habari za uwezeshaji.