Sisi ni Nani
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa na Sheria ya 16 ya 2004 kama njia ya kuharakisha mchakato wa kuwawezesha Watanzania kiuchumi. Baraza ina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia na kutathmini na pia kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini. Pia inajukumu la kuhamasisha rasilimali na kusimamia fedha maalum kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji wa kiuchumi. Uwezeshaji wa Kiuchumi ni moja ya njia ya kufikia MKUKUTA, MDG na hatimaye ndoto ya kitaifa ya mwaka 2025.
Tangu uhuru, Tanzania imejaribu kutengeneza na kupitisha sera kadhaa na mikakati ambayo inalenga kuendeleza Taifa na kuwawezesha watu wake kushiriki katika usimamizi wa uchumi wao. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Azimio la Arusha, Ungatuaji wa majukumu ya serikali kwa kupeleka madaraka mikoani,Biashara Huria, na Ubinafsishaji wa Makampuni ya Serikali. Ingawa sera hizi hazikufikia kikamilifu malengo yaliyokusudiwa, hata hivyo ilikuwa ni chachu ya kuleta maendeleo, amani, utulivu na umoja ambao ni mali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi.
Watumiaji wakuu wa huduma zetu ni makundi ya watu binafsi, vyama na vyama vya ushirika wanaohusika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi; utafiti na taasisi za kitaaluma; na idara za serikali.
NEEC inahamasisha rasilimali kutoka ndani na nje ya nchi na tunakaribisha washirika wenye nia ya kujiunga na jitihada zetu katika kufikia maono yenye heshima ya kuwawezesha Watanzania.