BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI LAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI
Imewekwa: 10 Oct, 2025
BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI LAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI LAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), limeendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es salaam katika ukumbi wa hoteli ya Peacock.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza, Bibi Neema Mwakatobe yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kazi zinazofanywa na Baraza katika usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mtendaji alisema kwamba Baraza linatarajia kuendeleza mshikamamo na vyombo vya habari lakini pia litaendelea kutoa mafunzo ili kuhakikisha kila fursa iliyopo inawafikia wananchi.
Nae Katibu wa Chama cha waandishi wa habari Tanzania, ndugu Seleman Msuya alishukuru uongozi wa Baraza kwa fursa ya mafunzo na kuwaomba kuendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa mikoa mingine ili na wao waweze kuzitangaza fursa zinazopatikana katika Baraza. 
Miongoni mwa watoa mada wakati wa mafunzo hayo ni pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi ndugu Gwakisa Bapala,Kaimu  Mkurugenzi wa uwezeshaji na ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkatati, Ndugu Siraji Nalikame na Mwanasheria Emmanuel Kalengela.
Maafisa hao kutoka Baraza la la Uwezeshaji waliwasilisha mada za Mifuko ya uwezeshaji,ushiriki wa Watanzania katika uchumi,utoaji wa huduma za biashara,wasilisho la mabadiliko ya sheria, wasilisho kuhusu Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumni na muongozo wa watoa huduma za biashara.
Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mtendaji aliwashukuru waandishi kwa kujitokeza kwao na ushirikiano waliouonesha muda wote wa mafunzo na kuahidi kufanyia kazi maoni yote yaliyowasilishwa.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo